Mamlaka inayoshughulika na wanyamapori nchini Kenya, Kenya Wildlife Service (KWS) imeamua kuwaweka vifaa vya kuwafuatilia Simba waliopo kwenye mbuga ya wanyama pori iliyopo kwenye viunga vya jiji la Nairobi.

Hatua hiyo ya KWS imekuja kufuatia matukio kadhaa ya wanyama hao kutoroka kwenye mbuga hiyo na kuingia mitaani hivyo kuhatarisha maisha ya binadamu na mali zao.

Hadi sasa KWS wana Simba sita ambao wamewekwa vifaa hivyo vilivyounganishwa na Satellite asa wamemdunga Simba mmoja kifaa hicho miongoni mwa Simba 36 waliopo kwenye hifadhi hiyo lakini zoezi hilo linatarajiwa kuendelea kwa Simba wote waliopo kwenye hifadhi hiyo.

Mbuga hiyo iliyoanzishwa mwaka 1946 imeendela kuvamiwa na makazi ya binadamu huku ujenzi wa maghorofa ukipelekea watu kuwaona wanyama waliofungiwa kwenye uzio.

Hatua hiyo pia imechangiwa na kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Simba mmoja mwaka jana na askari wa wanyapori baada ya kutoka nje ya mbuga na kuanza kuzurura mitaani huku Simba mwingine akiuawa kwa kuchomwa mshale kusini mwa Nairobi.

Wataalamu wa mazingira wamedai kuwa kitendo cha reli ya treni kupitishwa katikati ya mbuga hiyo kimeathiri tabia ya wanyama na kuwafanya Simba watafute mahali penye utulivu na ukimya zaidi kwaajili ya uwindaji wao.

Kenya inakadiriwa kusalia na Simba 2,000 tu.

kenyan-wildlife-services

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *