Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa tahadhari kufuatia ripoti inayoonyesha kuwa huenda watoto wengi wanachukuliwa kujiunga na wapiganaji wa al-Shabab nchini Somalia.

Pamoja na watoto hao kufundishwa matumizi ya silaha za kivita pamoja na kushirikishwa kwenye mapambano lakini pia Guterres amedai kuwa hufundishwa kuwa wapelelezi, kusafirisha silaha na kufanya kazi za ndani.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya nusu ya wapiganaji wa al-Shabab ni watoto huku angalau asilimia 60 ya vitu vilivyokamatwa Machi 2016 kwenye eneo la Puntland vilikuwa vya watoto.

Mkuu huyo amedai kuwa watoto wengi wamelaghaiwa kwa ahadi za kusomeshwa pamoja na kupatiwa ajira.

Hata hivyo licha ya Guterres kulitaja kundi la al-Shabab kuwa kinara wa kutumia watoto kama wanajeshi lakini pia amelitaja jeshi la nchi ya Somali kuwa nalo linaajiri na kuwatumia askari watoto.

Ripoti hiyo indai kuwa imethibitika kuwa watoto 6,163 (5,993 wavulana na 230 wasichana) walitekwa na kuingizwa kwenye majeshi kuanzia Aprili 1, 2010 hadi Julai 31, 2016 ambapo zaidi asilimia 30 ya matukio hayo ikitokea mwaka 2012.

Kundi la Al-Shabab linadaiwa kuongoza kwenye utekaji huo ambapo zaidi ya asilimia 70 ya matukio hayo sawa na utekaji wa watoto 4,213 yalithibitika kufanywa na kundi hilo.

Jeshi la Serikali linadaiwa kuteka watoto 920 katika kipindi hicho hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *