Klabu ya Manchester United imeshika nafasi ya kwanza kwa kujiingizia kipato kikubwa msimu uliopita baada ya kujikusanyia Euro milioni 689 msimu wa 2015-2016.
Manchester United imeipiku Real Madrid baada ya kufanya vizuri katika michezo kwa miaka 11baaada ya kukusanya kipato kikubwa takribani Euro milioni 689 katika msimu wa 2015-2016.
Ukijumlisha vipato vya timu ishirini bora kwa msimu wa 2015-2016 vimeongezeka kwa asilimia 12% na kufikia euro billioni 7.4 hii haijawahi kutokea kwa ligi ya Uingereza.
Hii ni mara ya kwanza kwa Manchester United kushikilia nafasi hiyo baada ya kufanya hivyo msimu wa 2003-04.
Klabu ya Real Madrid wameshuka mpaka nafasi ya tatu wakiacha na Barcelona iliyoshika nafasi ya pili baada ya kujikusanyia Euro 620.2.
Orodha ya timu 10 zilizoingiza mapato makubwa 2015-2016
1 Manchester United 689
2 Barcelona 620.2
3 Real Madrid 620.1
4 Bayern Munich 592
5 Manchester City 524.9
6 Paris St-Germain 520.9
7 Arsenal 468.5
8 Chelsea 447.4
9 Liverpool 403.8
10 Juventus 341.1