Rais wa Marekani, Barrack Obama amebatilisha kifungo cha mwanajeshi wa nchi hiyo Chelsea Manning aliyehukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kufichua nyaraka za siri.

Taarifa kutoka ikulu ya White House zinasema kuwa Manning ataachiwa huru ifikapo mwezi wa tano mwaka huu.

Mwanajeshi huyo aliyekuwa mwanamageuzi alifanya kazi Iraq alikuwa akijulikana pia kama Bradley Manning.

Alikutwa na hatia hiyo mwaka 2013 kwa kuweka hadharani nyaraka za siri za kijeshi na kidiplomasia katika tovuti ya WikiLeaks.

Pia rais Obama ametoa msamaha kwa mstaafu Generali James Cartwright aliyekubali kosa la kutoa taarifa za uongo katika uchunguzi uliokuwa ukifanywa na FBI katika udukuzi wa compyuta kuhusu mipango ya kinyuklia ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *