Timu ya taifa ya Uganda ‘Cranes’ leo inatupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya mataifa ya Afrika ‘Afcon’ dhidi ya Ghana.

Uganda wanaingia katika michuano hiyo tokea mwaka 1978 walipopoteza dhidi ya Ghana katika hatua ya fainali lakini wakati huu wanaingia wakiwa ndio timu bora ya Afrika 2016.

Katika mchezo wa mwisho kwa timu hizi kukutana zilitoka suluhu ya 0-0 na hapa ilikuwa kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 nchini Urusi.

Ghana nao wanataka kushinda kombe hili ambalo hawajalipata tokea mwaka 1982 hadi sasa hawajashinda tena.

Mafanikio makubwa kwa Uganda katika michuano hii ni ushindi wa pili miaka 39 iliyopita ambapo sasa wamepata nafasi hiyo.

Ghana ni ya nane barani Afrika na ya 54 duniani wakati Uganda inashika nafasi ya 18 Afrika ya ya 73 duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *