Beki wa Liverpool, Joel Matip atakosa mechi sita au zaidi za klabu yake baada ya kukataa kujiunga na timu ya taifa ya Cameroon kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Gabon.
Matip amekataa kujiunga na timu ya Taifa ya Cameroon baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 25 amecheza mechi 14 msimu huu na mwisho kucheza Cameroon ilikuwa Septemba 25 mwaka 2015.
Shirikisho la soka la kimataifa Fifa limesema kuwa Matib amekacha kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon bila ruhusa kwa hiyo hatocheza Liverpool mpaka Cameroon itakapotoka kwenye michuano hiyo.
Mechi atakazokosa beki huyo ni mechi ya raundi ya tatu ya michuano ya FA dhidi ya Playmouth, mechi ya ligi kuu dhidi ya Swansea City, nusu fainali ya kombe EFL dhidi ya Southampot pamoja mechi za ligi kuu dhidi ya Hull City na Chelsea.
Kama Cameroon itafanikiwa kufika fainali kwenye mashindano hayo ya Afcon Februari 5 beki huyo pia atakosa mechi ya Liverpool dhidi ya Tottenham itakayofanyika katika uwanja wa Anfield Februari 11.