Mkali wa hip hop Bongo, Nikki wa Pili amesema kuwa migogoro ya wakulima na wafugaji inayoendelea nchini inasababishwa na wafugaji kupora ardhi yao katika maeneo tofuti na baadhi ya viongozi.
Nikki wa Pili amesema kuwa mara nyingi wafugaji jamii ya wamasai ambao wanapigana na wakulima katika maeneo mbalimbali nchini ni kutokana na wafugaji hao kuporwa ardhi katika maeneo ya Longido, Serengeti na maeneo mengine.
Staa huyo kutoka kundi la Weusi ameadai kuwa kutokana na kitendo cha majaji na viongozi mbalimbali kuhodhi maeneo makubwa ya ardhi Morogoro ndiyo kunapelekea vita kubwa kati ya wakulima na wafugaji mkoani humo mpaka kupelekea kuuana.
Nikki wa Pili amesema kuwa kutokana na kitendo cha viongozi na watu wenye pesa kuchukua maeneo makubwa makubwa na kuwaacha wanyonge wakiwa na vieneo vidogo ndiyo chanzo cha migogoro hiyo.
Kauli hiyo ya Nikki wa Pili imekuja kufuatia kukithiri vitendo vya migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji mpaka kupelekea watu kuaga dunia au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na migogoro hiyo.