Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeghairisha kesi inayowakabili wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambao wanadaiwa kumfanyia shambulio la kudhuru mwili katibu tawala wa mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.
Wabunge wanaokabiliwa na kesi hiyo ni, Halima Mdee wa Kawe, Mwita Waitara wa Ukonga na Saed Kubenea wa Ubungo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyofunguliwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, inadaiwa kuwa wabunge hao pamoja na makada kadhaa wa Chadema, walifanya tukio hilo Februari 27, mwaka jana wakati Mmbando akisimamia mkutano wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Awali, kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi, Wakili wa Utetezi, Fredrick Kihwelo huku wakili wa serikali akiwa ni Diana Lukundo.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Februari 13, mwaka huu itakaposikilizwa tena