Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametetea uamuzi wake wa kuchezesha kikosi cha umri mdogo zaidi katika mechi ya Kombe ya FA ambayo walitoka sare 0-0 na Plymouth.
Klabu hiyo sasa inalazimika kusafiri Devon kwa mchezo wa marudiano.
Huu ni mzigo ikizingatiwa kwamba klabu hiyo sasa itatakiwa kucheza mechi sita Januari.
Liverpool watakutana na Southampton kwenye mechi mbili nusufainali ya Kombe la EFL na wana mechi za Ligi ya Premia dhidi ya Manchester United, Swansea na Chelsea.
Hata hivyo kocha raia wa Ujerumani amesema hafikiri kwamba alikosea kwenye uamuzi wake.
Wachezaji waliochezeshwa Jumapili walikuwa na umri wa kadiri wa miaka 21 na siku 296 ambao hawana uzoefu na mechi.
Mshambuliaji Ben Woodburn, 17, ndiye mfungaji mabao wa umri mdogo zaidi Liverpool baada yake kuifunga Leeds Kombe la EFL mapema msimu huu, na ni miongoni mwa waliokuwa kikosini.