Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad  amesema kuwa kimya chake kinamaana na siyo kama baadhi ya wanasiasa wanavyosema.

Kauli hiyo ameitoa jana mjini Unguja, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, ambapo pamoja na mambo mengine alisema umaskini sasa umekuwa ukiwatesa wananchi katika kila eneo.

Katika uchaguzi huo CUF inawakilishwa na mgombea wake Abdulrazak Khatib Ramadhan ambaye anapambana vikali na mgombea wa CCM, Juma Ali Juma.

Maalim Seif ni kama alikuwa akijibu mapigo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdurhamn Kinana ambaye mwishoni mwa wiki alisema kuwa kiongozi huyo anazungumza hali ya kuwa hajui lolote kinachoendelea katika nchi wala katika chama chake.

Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Hafidh Tahir aliyefariki dunia wakati akihudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma mwezi Novemba mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *