Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Mtwara wamkamata magari mawili yenye magunia ya korosho 350 sawa na tani 29 baada ya kubainika mihuri iliyotumika kwenye vibali ni ya kughushi.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara, Mhandisi Juma Kisaura alimesema mzigo huo ulitiliwa shaka hali ambayo ililazimu askari wa bandari hiyo kuomba vibali ambavyo pia vilitiwa shaka.

Amesema mzigo huo, uliokuwa umepelekwa bandarini hapo kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi, ulisimama kwa muda ili  taratibu za ndani ya Bandari zifanyike.

Kwa upande wke Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego amesema wafanyabiashara wanatakiwa kuwa makini kwa kuwa mkoa huo umejipanga vizuri kukomesha uuzwaji wa korosho kwa njia haramu.

Amesema upo mpango kabambe wa kuhakikisha wakulima wa korosho,wanapata stahiki zao vizuri bila kuwaruhusu wafanyabiashara wajanja wajanja kuwarubuni.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *