Wafungwa 55 wamepoteza maisha katika vurugu zilizotokea katika gereza nje ya mji wa Manaus nchini Brazil.

Vurugu hizo katika gereza la Anisio Jobim zilianza siku ya Jumapili na kuisha baada ya saa kumi na saba pindi wafungwa hao waliposalimu amri.

Mkuu wa usalama katika jimbo la Amazonas, Sergio Fontes amesema kuwa vurugu hizo zilikuwa zimepangwa muda mrefu.

Wafungwa waliweka bayana kwa uongozi wa gereza kwamba kila kitu kitakuwa sawa katika msimu huu wa sikukuu.

Fontes ameongeza kusema kuwa baadhi ya wafungwa walitoroka na wengine wameuawa hata hivyo, Idadi kubwa ya wafungwa waliokuwa wametoroka tayari wamekamatwa.

Nako nje ya gereza, ndugu wa wafungwa waliokusanyika walijawa na shauku ya kutaka kujua hali ya ndugu zao.

Mama wa mmoja ambae mwanae ni mfungwa ameonekana akishikilia gamba la risasi huku akisema polisi hawana nia ya kuwalinda wafungwa.

Maafisa wa gereza wamesema makundi hasimu yaliyopo nje na ndani ya gereza yamepigana kwa kutaka kuwa na sauti dhidi ya kundi jingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *