Tume ya Ushindani nchini (FCC) imeteketeza bidhaa mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 500, ikiwemo vifaa vya umeme kwa ajili ya transfoma.

Bidhaa hizo zikiwemo vifaa 1850 vya umeme kwa ajili ya kufungwa kwenye transfoma na njia za umeme vyenye thamani ya Sh milioni 231.2, vimekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini kufuatia misako iliyofanyika ya kutokomeza bidhaa bandia sokoni.

Ofisa Mwandamizi Mawasiliano na Mahusiano wa Tume hiyo, Frank Mdimi amesema bidhaa hizo zimekamatwa katika msako uliofanywa katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Dar es Salaam na maeneo mengine ikiwemo bandari zote.

Alizitaja bidhaa zilizokamatwa na thamani yake kwenye mabano ni miswaki katoni 200 (Sh milioni 96), mafuta ya karafuu chupa 100 (Sh 300,000), nyembe za Gillette katoni 13 zenye paketi 1728 (Sh milioni 2.6), viatu aina ya Timberland na Caterpillar jozi 500 (Sh milioni 30).

Bidhaa zingine ni wino wa printa aina ya HP, kisha 704 (Sh milioni 126.7), betri za kompyuta mpakato 363 (Sh milioni 54.4), chaji za kompyuta mpakato 88 (Sh milioni 4) na vitabu vya kuandikia (Sh milioni 2) ambavyo jumla yake ni Sh 517,272,000.

Amesema mara nyingi walaji ndio wamekuwa wakidanganyika na wakati mwingine huko mahali pa kulalamika na kupata sehemu ya kutatua migogoro iwapo bidhaa itaharibika, kwa kuwa hatakuwa na mtu wa kumdai kwasababu bidhaa hizo zi za mwenye miliki bunifu husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *