Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linakutana na kufanya mazungumzo na wasanii kabla ya kuzifungia nyimbo zao baada ya kukiuka maadili ya kazi za sanaa.

Hayo yamesemwa na waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye baada ya kuwepo kwa udhaifu katika sheria ambazo zinaliongoza BASATA.

Waziri Nape amedai kwa sasa baraza hilo linakutana na wasanii wakati wa kuzifungia kazi zao pale wanapokiuka maadili ya kazi za sanaa.

Waziri huyo amesema serikali ikirekebisha sheria za sanaa na kuwa rafiki kwa watumiaji anaamini sekta ya sanaa inaweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza pato la Taifa.

BASATA ni baraza la sanaa la Taifa lililopewa dhamana ya kuendeleza sanaa nchini ambalo lilikuwa linalaumiwa na baadhi ya wasanii kutokana nakuzifungia kazi zao kwa kukosa maadili ya kazi za sanaa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *