Wakala wa Christiano Ronaldo, Jorge Mendes amesema kuwa Real Madrid imekataa takriban pauni milioni 250 na klabu ya China ambayo haikutajwa jina ili kumnunua nyota wake Ronaldo.

Amesema kuwa nahodha huyo wa Portugal mwenye umri wa miaka 31 hana haja na mpango huo ambao ulishirikisha mshahara wa kila mwaka wa pauni milioni 85.

Ikumbukwe kuwa Ronaldo aliwahi kusema kuwa anaweza kucheza kwa miaka mingine 10 baada ya kusaini mkataba mpya na Real Madrid hadi Juni 2021.

Mendes amesema kuwa kama Ronaldo angenunuliwa na klabu hiyo angepokea kitita cha pauni milioni 1.6 kwa wiki ikiwa ni mara tatu ya zaidi ya kitita cha uhamisho wa pauni milioni 89 zilizogharimu uhamisho wa Paul Pogba kutoka Juventus kuelekea Manchester United.

Hatua hiyo inajiri baada ya klabu ya Shanghai Shenhua kutoka China kuthibitisha kwamba imemsajili Carlos Tevez kutoka klabu ya Boca Juniors.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *