Kesi ya mkurugenzi mkuu wa Jamii Forum, Maxence Melo imehairishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Januari 26 mwakani kutokana upelelezi kutokamilika.

Maxence Melo anashtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao na Kusajili tovuti ya JF kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Mashauri yote ya kesi hiyo yameahirishwa huku shauri la tovuti kutosajiliwa kwa kikoa cha .co.tz, Mheshimiwa Hakimu Simba anyaeendesha shauri hilo ameutaka upande wa Jamhuri kufanya upelelezi haraka kwa shauri hilo.

Maxence Melo, aliachiwa kwa dhamana Desemba 19, 2016 Mahakamani hapo baada ya kukaa lupango kwa siku kadhaa mpaka alipokidhi vigezo na masharti ya kudhaminiwa ambapo mahakama ilimtaka arudi leo kusikiliza kesi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *