Halmashauri ya wilaya ya Kindondoni imelipwa kiasi cha shilingi milioni 687 na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel ikiwa ni deni la kodi ya pango zilizokuwa zinazodaiwa na manispaa hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema fedha hizo zimelipwa baada ofisi yake kubaini mchezo mchafu uliokuwa umefanywa na watendaji wa halmashauri yake waliokuwepo huko nyuma ambao walificha mkataba kati yake na Zantel.
Hapi amesema kuwa fedha hizo zimelipwa Desemba 21 na mkataba huo wa zamani unaisha Januari mwakani.
Halmashauri hiyo imeamua kuelekeza fedha hizo ambayo ni sh 687,931,040 katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 40 katika halmashauri hiyo kwamba kama itaonekana inawezekana kujenga shule nyingine mpya ya sekondari.
Pia mkuu wa wilaya huyo ameipongeza Zantel kwa kutii maagizo waliyopewa na kulipa fedha hizo na tayari wamepewa risiti kuonesha kupokea fedha hizo na kwamba watu wote waliohusika katika jambo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.