Mwanamuziki wa Bongo fleva Dully Sykes amesema kuwa anatarajia kuanzisha lebo yake ya muziki kwa ajili ya kuinua vipaji vya wasanii pamoja na kukuza muziki wa Bongo fleva hapa nchini.

Dully Sykes ambaye alianza game ya muziki miaka ya tisini amesema kuwa ameamua kufungua lebo ili kuona muziki wa Tanzania unasonga mbele kimataifa tofauti na ilivyosasa ambapo wasanii wanaotamba kimataifa ni wachache kulinganisha na nchi kama Nigeria na Afrika Kusini.

Mkali huyo aliendelea kusema kuwa wasanii wa bongo wanaangushwa na uongozi wao kutokana na viongozi wao kutokuwa na malengo mazuri na wanamuziki hao huku akisema wasanii kama watakuwa na uongozi mzuri lazima wafike wanapotaka huku akitolea mfano menejimenti ya Alikiba chini Seven Mosha na Diamond chini Salaam SK.

Dully Sykes ni miongoni mwa wasanii wanaomiliki studio za muziki nchini ambapo anamiliki studio ya dhahabu records pamoja na studio 4.12 ambazo zote zipo chini yake japokuwa kwasasa hazifanyi vizuri kama hapo awali.

Kuhusu kujiunga na lebo nyingine kwasasa Dully Sykes amesema kuwa hana haja kujiunga na lebo nyingine yoyote ya muziki kwa kuwa na yeye ana mpango wa kuanzisha lebo yake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *