Maafisa wa Maliasili mkoani Ruvuma wanaushikilia mwili wa nyoka wa maajabu ambaye aliuawa na wananchi wenye hasira baada ya kumsababishia majeraha dereva wa bodaboda aliyekuwa amempakiza mmiliki wa nyoka huyo aliyekuwa pia amembeba nyoka huyo kwenye begi.
Nyoka huyo wa maajabu amezua gumzo mjini Ruvuma baada ya mmiliki wake kufariki dunia bila kuguswa na raia hao wenye hasira lakini alifariki dunia wakati nyoka huyo akishambuliwa na watu hao, na kabla ya raia hao kuanza kumshambulia nyoka huyo mmiliki huyo wa nyoka aliwasihi watu hao kuwa wakimuua nyoka huyo naye atakufa na kweli maeno yake yalitimia.
Mmiliki wa nyoka huyo, marehemu Denis Komba (26) alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa kwaajili ya matibabu lakini alifariki dunia.
Inadaiwa kuwa siku ya tukio Komba alikodi pikipiki (Bodaboda) ili impeleke nyumbani kwake lakini walipokuwa njiani dereva huyo wa Bodaboda, Kassian Haule (24) alihisi kutambaliwa na kitu mgongoni na alipogeuka ndipo alipomuona nyoka akiwa amesimamisha kichwa. Kassian aliruka kutoka juu ya pikipiki kisha kupiga mayowe ya kuomba msaada ambao uliwakusanya watu wengi waliotaka kujua kilichotokea na baada ya kusikiliza maelezo ya Kassian walianza kumsaka nyoka huyo aliyekimbilia kwenye mtaro wa maji taka.
Hata hivyo inadaiwa kuwa Komba aliwasihi sana watu hao wasimuue nyoka huyo kwani akiuawa nyoka huyo naye atakufa lakini maombi hayo hayakusikilizwa na ndipo watu walipoanza kumsahmbulia nyoka huyo hali iliyopelekea Komba kuanza kupoteza nguvu na kutokwa mapovu mdomoni.
Na baada ya kuuawa kwa nyoka huyo ndio Komba nae akiwa hana jeraha lolote alifariki dunia.