Aliyekuwa mfadhili wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia (Wazee wa Ngwasuma, Ndama Shaaaban Hussein ‘Pedeshee’ leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Ndama anatuhumiwa kutenda makosa sita ukiwemo utapeli wa Dola za Marekani 540, 390 ambazo ni sawa na zaidi ya Shilingi bilioni moja za T Awali kesi yake ilipopanda mahakamani hapo alisomewa mashtaka sita mbele ya Hakimu Victoria Nongwa na Mwendesha Mashtaka, Leonard Msigwa, akisaidiana na Christopher Challo kuwa mnamo Februari 20, 2014 mkoani Dar es Salaam, Ndama alitengeneza nyaraka feki zikionyesha kupata kibali cha kusafirisha sampuli za madini ya dhahabu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
Mashitaka ya pili, tatu na nne pia yalikuwa ya kugushi nyaraka, ikiwemo iliyotoka Umoja wa Mataifa iliyodai kuisafisha kampuni yake ya Muru Platinum Tanzania Investment Company Ltd kuwa imeruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu.anzania.
Nyaraka hizo zililenga kuiaminisha Kampuni ya Trade TJL DTYL Ltd ya Australia kuwa Muru ni watu halali kwa biashara hiyo.
Anadaiwa pia ugushi nyaraka zilizoonyesha kuwa alilipa kiasi cha Dola 331, 200 sawa na Shilingi milioni 728 kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kama kodi ya kupitisha mzigo huo hapa nchini.
Shitaka la tano ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Dola 540,390 kutoka kampuni hiyo ya Australia zilizowekwa katika akaunti ya Kampuni ya Muru katika Benki ya Stanbic, na shtaka la sita lilihusu utakatishaji wa fedha hizo.
Ndama alikana mashtaka yote akarudishwa rumande.
Kesi hiyo imeghairishwa mpaka Januari 6, 2017 kutokana na upelelezi wa polisi kutokamilika.
Picha kwa hisani ya Glaobal Publishers