Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepiga marufuku kwa kumbi za starehe nchini kupiga disko “disko toto”  kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

Taarifa ya Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza imesema kuwa uzoefu unaonesha kwamba nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuandaa madisko ya watoto hali ambayo imekuwa ikisababisha maafa.

Vile vile taarifa imesema baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuendekeza faida pasipokujali maelekezo ya vibali vyao.

Taarifa hiyo ilisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo hayo.

Baraza hilo limewataka wamiliki wa kumbi za starehe kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *