Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imehudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Mcheche Masaju na Viongozi wengine mbalimbali.
Walioapishwa ni Mhe. Mhe. Jaji Semistocles Simon Kaijage aliyeapishwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid aliyeapishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Harold Reginald Nsekela aliyeapishwa kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Kwa upande wa Majaji walioapishwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye, Mhe. Jaji Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi na Mhe. Jaji Dkt. Gerald Alex Mbonimpa Ndika, Mhe. Jaji Jackobs Casthom Mwatebela Mwambegele.