Idadi ya wanamuziki nchini Marekani wanaokataa ofa ya kutumbuiza kwenye sherehe ya kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani, Donald Trump imeongezeka baada ya mwanamuziki mkongwe Celine Dion kukataa ofa hiyo.

Uongozi wa mwanamuziki huyo  umesema kuwa Celine Dion hawezi kuhudhuria sherehe hizo kutokana na ratiba zake za show kumbana mkali huyo.

Mwanamuziki huyo alikuwa miongoni mwa wanamuziki waliotakiwa kutumbuiza kwenye sherehe za kuapishwa Trump zitakazofanyika Januari 20 mwakani kakini ameipiga teke ofa hiyo kwa madai kuwa siku hiyo atakuwa na show katika ukumbi wa Caesars Palace katika mji wa Las Vegas.

Celine Dion anaungana  na msanii Elton John ambaye naye alikataa ofa ya kutumbuiza kwenye sherehe hizo za kuapishwa kwa rais huyo mteule wa 45 nchini Marekani.

Wasanii wameonekana kutomuunga mkono Donald Trump kutokana na sera zake alizokuwa anataoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa Marekani uliofanyika mwezi uliopita na yeye kuibuka mshindi kwa kumpiku mpinzani wake Hillary Clinton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *