Jeshi la Polisi nchini limewapiga marufuku wamiliki wa nyumba za starehe kujaza watu kupita kiasi na kuwataka wazingatie uhalali wa matumizi ya kumbi zao na uwezo wa kumbi hizo katika kipindi cha sikukuu.

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa leo na Msemaji wake ACP Advera Bulimba kuelekea katika kipindi cha sikuu za Krismas na Mwaka Mpya, imesema kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba wananchi wanasherehekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu bila ya kuwepo kwa vitendo vya uhalifu.

Taarifa hiyo imesema kuwa ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya ya watu.

Aidha jeshi hilo limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na kuchukua hatua stahiki za haraka kwa kutoa taarifa kupitia kwa makamanda wa polisi wa miko pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu.

Pia amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao ili kuepuka upotevu wa watoto, ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *