Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Yanga na Azam wamepangiwa ratiba zao za mechi za awali katika michuano hiyo mikubwa kwa upande wa vilabu Barani Afrika.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) linaonyesha kuwa Mabingwa wa Tanzania bara tumu ya Yanga itaanza mechi ya kwanza dhidi ya tmu ya Ngaya de Mbe kutoka visiwa vya Comoro.

Kwa upande wa Azam FC ambao wao ushiriki kombe la Shirikisho Afrika itaanza kampeni yake dhidi ya timu ya mshindi kati ya Mbabane Swallows ya Swaziland na Opara United ya Botswana.

Yanga wataanzia Februari 10 hadi 12 kabla ya marudiano Februari 17 hadi 19, mwaka huu.

Azam wao wataanzia nyumbani Machi 10 hadi 12 na marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.

Yanga wakivuka hatua hiyo watakutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia au APR ya Rwanda katika Raundi ya kwanza.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *