Daktari bingwa wa magonjwa ya ubongo na mishipa katika Kitengo cha Mishipa ya Fahamu (Neurology) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Patience Njenje amesema kuwa maderva wa piki piki (Boda boda) wapo hatarini kuharibikiwa mfumo wa fahamu, kupooza na kupata kifafa miaka ijayo.

Dk Njenje amesema kuwa hali hiyo inachochewa zaidi na ongezeko la matukio ya ajali ambazo wamekuwa wakizipata kila siku wakiwa barabarani.

Dk. Njenje ameongeza kwa kusema kuwa matatizo ya ubongo kitaalamu hugawanywa katika makundi mawili, ‘organic’ yaani nyama ya ubongo na ‘in-organic’ yaani utendaji wa ubongo.

Pia Dki huyo amesema kuwa wanawake wanaotumia dawa za nywele nao hujiweka katika hatari kwani nyingi huenda kuharibu mfumo wa ubongo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *