Nahodha wa Yanga, Haruna Niyonzima amesema kuwa wachezaji wa timu wamegoma kufanya mazoezi ili kuushawishi uongozi waweze kuwalipa mishahara yao ili kuweza kujikimu kimaisha.

Nahodha huyo amesema maisha yamekuwa magumu na wao wanategemea mishahara yao ili kuweza kupata huduma mbalimbali hivyo kufanya hivyo wanaamini uongozi wa Yanga utawasikiliza na kulipatia ufumbuzi haraka.

Amesema uongozi unapaswa kuangalia kilichopo mbele yao ambapo timu yao inakabiliwa na ushindani mkali wa kupigania ubingwa kati yao na wapinzani wao Simba hivyo nivyema wakawaanda kisaikolojia wachezaji ili waweze kupambana katia mechi zao kuliko kufanya hivyo.

Kwaupande wake Kamaimu Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga Baraka Desidediti amesema kwasasa wapo katika mchakato wa kulifanyia kazi hilo na muda siyo mrefu watamaliza tatizo hilo la kuchelewa kwa mishahara.

Yanga wanatarajia kushuka dimbani Ijumaa ya wiki hii kupambana na African Lyon, katika mchezo wa pili wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *