Mfanyabiashara Charles Kijangwa hakumiwa kwenda jela miaka 35 na kulipa faini ya sh bilioni 3.7 na mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga kwa kosa la kujihusisha na biashara ya meno ya tembo.

Mtuhumiwa huyo amehukumiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cresencia Kisongo, baada ya kuruka dhamana kwa miaka sita.

Mshtakiwa huyo alikabidhiwa mahakamani hapo baada ya kukamatwa na askari wa kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Mashariki na Pwani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Lushoto.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Saraji Iboru, alidai mahakamani kuwa mshtakiwa Kijangwa alikuwa akitafutwa na Serikali kwa muda mrefu tangu mwaka 2010 baada ya kuruka dhamana katika shauri la uhujumu uchumi namba 6/2007.

Mshtakiwa alishtakiwa na wenzake Michael Msuya na Nyaisa Makori ambao walitiwa hatiani na mahakama, wakahukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kosa la kumiliki kilo 5,000 za meno ya tembo kwa shtaka la kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *