Rais mteule wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa nchi hiyo inatakiwa kuiomba China kuiweka manuwari ya Marekani iliopatikana katika bahari ya kusini mwa taifa hilo.

Awali Trump alikuwa ameishutumu Beijing kwa kuiba manuwari hiyo katika maji ya kimataifa.

China iliichukua manuwari hiyo katika pwani ya Ufilipino wakati meli za wanamaji wa Marekani zilipojaribu kuichukua, hatua ilioikasirisha Marekani.

China imesema kuwa itaikabidhi Marekani, lakini matamshi ya Trump huenda yakatatiza mpango huo.

Wakati huohuo Trump amekamilisha ziara yake ya wiki tatu ya kusherehekea ushindi , katika mji ulioshuhudia mkutano mkubwa zaidi wakati wa kampeni zake.

Alipowasili katika mji wa Mobile, Alabama, Trump alikaribishwa na kundi la wanawake waliovalia mavazi ya kitamaduni yanayovaliwa na jamii za kusini mwa Marekani.

Katika uwanja uliojaa pomoni, Trump aliahidi kwamba atatimiza ahadi yake ya kujenga ukuta kwenye mpaka wa Mexico na Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *