Dunia haiishi maajabu……….
Utafiti unaondelea kufanywa nchini Uingereza na wataalamu wa ugonjwa wa kisukari (diabetes) umeanza kuonyesha dalili chanya kuwa mbwa anaweza kumsaidia mgonjwa wa Sukari kutambua hali ya hatari kwenye mail wake katakana na kushuka kwa kiwango chake cha sukari.
Utafiti huo wa awali umebainisha kuwa mbwa huweza kunusa ongezeko la harufu fulani kutoka katika mwili wa mgonjwa katika kipindi cha siku moja au usiku mmoja ambayo ni usher ya kushuka kwa sukari kwenye mail wa mtu huyo kabla ya mgonjwa huyo kujisikia hali ya kutetemeka, kuchanganyikiwa na wakati mwingine kupoteza fahamu.
Mbwa hao ambao hupewa mafunzo maalum wanajulikana kwa jina na Labrador na huweza kumuashiria mgonjwa kuwa hali ya hatari iko mbele yake hivyo achukue hatua za kukabiliana nayo.
Mpaka sasa utafiti huo unafanywa kwa wagonjwa wa sukari wenye aina ya kisukari ijulikanayo kama: Kisukari aina ya kwanza (Type 1 diabetes).
Ni vyema wataalamu wa nchini wakafuatilia utafiti huu ili kuweza kuwasaidia wagonjwa waliopo nchini.