Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema kuwa uhenda akagombea urais nchini Korea Kusini baada ya kumaliza muda wake kama katibu mkuu wa UN.
Muhula wake Ban kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa unakamilika mwisho wa mwezi huu wa Disemba
Wakati wa mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari, Ban alisema kuwa baada ya kupata mapumziko anarudi nchini mwake Korea Kusini kuona vile ataisaidia nchi yake.
Uchaguzi wa uraia nchini Korea Kusini unatarajiwa kufanyika Desemba mwaka 2017 kutokana na katiba ya nchi hiyo.
Lakini huenda uchaguzi huo ukafanyika katika muda wa miezi miwili baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura ya kumuondoa madarakani Rais Park Geun-hye, kutokana na sakata, ambapo analaumiwa kwa kumruhusu rafiki wake wa karibu kunufaika kifedha.
Ikiwa mahakama ya katiba itadumisha kura hiyo ya kumuondoa, atakuwa rais wa kwanza wa Korea Kusini aliye madarakani kuondelwa katika kipindi cha uhuru wa nchi hiyo.