Jaji Mkuu Mohammed Othman Chande amesema ndani ya mwaka mmoja wamepokea malalamiko 71 kuhusu mawakili yakiwamo ya kutoa siri za wateja.
Amesema hayo jana katika hafla ya kuwaapisha mawakili wapya 287. Idadi hiyo imefikisha jumla ya mawakili kufikia 6,082.
Amesema miongoni mwa malalamiko yaliyowasilishwa ni kutetea wateja chini ya kiwango, kushindwa kutunza siri za wateja.
Pia Jaji Chande amewataka mawakili kuisaidia mahakama kuondoa mlundikano wa kesi na waziendeshe kwa gharama inayoridhisha.
Kwa upande wake Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali amewataka washiriki katika kutoa haki, wawe waaminifu kwa mahakama na wateja kwani wakienda kinyume haki itapotea.
Jaji Wambali amewataka mawakili hao wapya kufika maeneo ya nje ya mji ili wasaidie upatikanaji wa haki.