Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza jitihada zilizoachwa na Serikali za awamu zilizopita ili kuzidi kuwaletea maendeleo Watanzania.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara yaliyofanyika katika uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli alisema ku wa Serikali ya Awamu ya Tano imeanza jitihada za kuboresha huduma za maendeleo ya jamii, ambapo katika bajeti ya mwaka 2016/17 imeamua kutenga asilimia 40 ya bajeti katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo umeme, miundombinu, afya, elimu.

Rais Magufuli alisema juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali ni kuboresha maslahi kwa watanzania kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuwawajibisha wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli aliwataka watanzania kudumisha amani na kulinda muungano uliyopo kwani amani ni msingi wa maendeleo ya nchi bila amani hakuna maendeleo. R

ais Magufuli pia alitoa wito kwa wantanzania kuendelea kufanya kazi kiwa bidii kwani kila mwananchi ana haki ya kufanya kazi, na kusema kuwa waasisi wa nchi walileta uhuru kwa maendeleo ya nchi kwani Uhuru ni kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *