Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema itaruhusiwa mikutano ya kisiasa wakati wa kampeni za uchaguzi katika Jimbo la Dimani Zanzibar na kata 22 ambazo zitafanya uchaguzi wa madiwani.

Tume hiyo imesema itatumia Sh bilioni 3.9 kama gharama za uchaguzi katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na kata 22 ambazo zitafanya uchaguzi wa madiwani.

Uchaguzi wa Jimbo la Dimani utagharimu Sh bilioni 1.7 na ule wa kata 22 unatarajia kugharimu Sh bilioni 2.2.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Ramadhani Kailima amesema uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Dimani, Zanzibar unafanyika kutokana na kifo cha Mbunge wa jimbo hilo, Hafidh Ali Tahir aliyefariki alfajiri ya kuamkia Novemba 11, mwaka huu kwenye Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wa Chama cha Wananchi amesema Kipengele cha 4(5) (iii) kinasema fomu za wagombea kwenye chama chenye mgogoro zisainiwe na viongozi wakuu wote wawili kwa vile wamethibitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Amesema kama CUF ina mgogoro mgombea atakayependekezwa atatakiwa kupitisha fomu zake na kusainiwa na viongozi wote wawili wea chama hicho kutokana na kutambulika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *