Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), kuwasimamisha kazi maofisa waandamizi watano wa mfuko huo.

Maofisa hao ni wanaosimamia mpango huo pamoja na Meneja wa Uratibu na Mkurugenzi wa Uratibu kutokana na kushindwa kusimamia mpango wa kunusuru kaya masikini.

Kairuki alisema maofisa hao ndio viongozi wasimamizi wakuu wa mpango huo katika Awamu ya Tatu ya Tasaf na wamesimamishwa kupisha uchunguzi wa jinsi walivyohusika kuvuruga utekelezaji wa mpango huo hadi kufikia kuandikisha kaya zisizo na sifa ufanyike.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Kairuki alisema ameshauriana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na tayari ameshaelekeza waratibu wa Tasaf wa wilaya pia wasimamishwe kazi.

Aidha amesema ameagiza ufanyike uchunguzi wa kina kubaini ushiriki wa maofisa hao na kuchukua hatua stahiki kwa wale watakaothibitika kuhusika.

Aidha ametaka uchunguzi huo ukamilike ndani ya mwezi. Karuki alisema baada ya uhakiki kufanyika kaya 55,692 zimeondolewa kwenye mpango kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo, kaya kuhama kijiji, kutojitokeza mara tatu mfululizo kupokea ruzuku, kuwa wajumbe wa kamati mbalimbali, wastaafu, viongozi na watumishi wa umma.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *