Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali imetenga Sh trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji vyote vilivyopo nchini.
Waziri mkuu ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Mto wa Mbu Wilayani Monduli Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali imetenga fedha hizo kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme kwa wananchi wake.
Pia amesema wazabuni watasaini mikataba yao ya kufanya kazi hiyo ya usambazaji wa umeme vijijini Desemba 15 mwaka huu na kazi kuanza mara moja ili kufungua fursa za ajira katika sekta mbalimbali nchini.