Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandala ameongozewa kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa chuo hicho.

Uamuzi huo umekuja baada ya mkuu wa chuo hicho, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete kufanya mashauriano na rais John Pombe Magufuli kumuongezea muda Mukandala ambaye muda wake ulimalizika Disemba 4 mwaka huu.

Profesa Mukandala aliteuliwa kwa kipindi cha sasa cha miaka mitano kilichoanza Desemba 5, 2011 na kumalizika Desemba 4, mwaka huu.

Baada ya kuongezewa muda huo, Profesa Mukandala amesema kuwa alikuwa tayari ameshajitayarisha kwamba juzi angekabidhi madaraka hayo kwa mtu mwingine, lakini kwa imani waliyokuwa nayo uongozi wa chuo hicho uliridhia aendelee kwa mwaka mwingine.

Amewashukuru waliomchagua na ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wote na jumuiya ya wanachuo ili Udsm iendelee kuwa bora. Pia alisema ataendelea kuenzi na kutunza tunu ya chuo hicho iliyoachwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma (UDASA), Dk George Kahangwa amesema kuna mambo mengi Profesa Mukandala alikuwa bado anayafanyia kazi hayajakamilika, hivyo wakati anamalizia kipindi chake, ikatokea akachaguliwa mkuu mpya wa chuo hicho Kikwete.

Dk Kahangwa amesema hivyo inabidi akamilishe mambo yaliyo mezani kwake wakati wamempata mkuu mpya wa chuo Jakaya Kikwete.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *