Muigizaji wa Bongo movie, Gabo Zigamba amesema kinachoikwamisha tasnia ya filamu nchini ni kukosa umoja kwa wasanii kiasi cha kukubali kupelekwa pelekwa kama nyumbu.

Gabo amesema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akijibu maswali ya wanafunzi wa UDSM, katika kampeni ya ‘Ready To Work’ inayoendeshwa na Benki ya barclays ikiwa na lengo la kukabiliana na tatizo la ajira.

Gabo amesema endapo wasanii wataamua kuwa na umoja wenye nguvu, hakuna kitakachoharibika, na tasnia hiyo itapiga hatua kwa kiasi kikubwa kama ajira rasmi.

Pia Gabo amesema kilichomfikisha hapo ni matumizi mauri ya akili zake na kwamba hakuna mtu yeyote aliyemsaidia huku akiwaasa wasanii wengine kuwa na matumizi mazuri ya akili zao ili kuisukuma mbele tasnia hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *