Klabu ya Azam FC inatarajiwa kwenda visiwani Zanzibar siku ya jumatano kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Desemba 17, mwaka huu.

Timu hiyo ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa nafasi ya tatu na pointi 25, imedhamiria kufanya kweli mzunguko wa pili huku ikifanya usajili wa maana kwa kuwanyakua Waghana watatu, Enock Atta Agyei, Yahaya Mohammed na Samuel Afful.

Meneja wa timu hiyo, Philip Alando, amesemakuwa kikosi chao rasmi kitaanza mazoezi huku keshokutwa Jumatano wakitarajiwa kwenda visiwani humo.

Klabu hiyo imezamilia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kupata matokeo mabovu katika mzunguko wa kwanza na kuambulia alama 25 ikishika nafasi ya tatu nyumba ya Simba na Yanga.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *