Marekani imeipa Kenya helikopta mpya sita ambazo zitatumiwa kwenye vita dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia.
Ndege mbili zaidi za helikopta aina ya Huey II, zitatolewa kwa Kenya mwezi Mei.
Waziri wa ulinzi nchini Kenya Raychelle Omamo anasema kuwa ndege hizo zitatumiwa kuendesha oparesheni ngumu hasa nchini Somalia.
Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec, amesema kuwa huo ndio msaada mkubwa zaidi kuwai kutolewa na Marekani kwa nchi moja Kusini mwa jangwa la Sahara.
Helikopta hizo zitatumiwa kwenye vita na pia katika shughuli za uokoaji.