Mfalme, Charles Wesley Mumbere kutoka magharibi mwa Uganda amefunguliwa mashtaka ya mauaji kufuatia mapigano ya mwishoni mwa wiki ambapo watu 62 waliuawa.
Anatawala katika ufalme ya kitamaduni kwenye milima ya Rwenzori umbali wa kilomita 340 kutoka magharibi mwa mji mkuu Kampala.
Wafuasi wake ambao ni jamii ya Bakonzo wamesambaa kutoka nchini Uganda hadi nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Mizozo ya ardhi imesababisha migawanyiko kuhusu mipango ya kuigawanya kasese, moja ya wilaya saba zilizo eneo la Rwenzori.
Mfalme Mumbere na baadhi ya wafuasi wake wamelaumiwa kwa kupanga kubuni vuguvugu la kujitenga na kuunda taifa jipya kwa jina Yiira.
Charles Mumbere alitawazwa kuwa mfalme wa Rwenzururu mwaka 2009, bbada ya kuishi na kufanya kazi nchini Marekani kwa miaka mingi.