Rais wa Zambia, Edgar Lungu ameondoka nchini baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu baada ya kufanya mazungumzo na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kuhusu kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Katika ziara yake hiyo rais Lungu alitembelea mamlaka ya reli Tanzania na Zambia, TAZARA na kuwahakikishia wafanyakazi kuwa Zambia itafanya jitihada zote kuhakikisha inatatua changamoto za uendeshaji.
Rais Lungu alikutana na Rais Dkt John Magufuli kuzungumzia mipango mbalimbali ya maendeleo na kusisistiza kuendeleza ushirikiano ulioanzishwa na waasisi wa mataifa hayo akiwemo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Keneth Kaunda wa Zambia.
Pia rais huyo ametembelea mabomba ya kusafirishia mafuta TAZAMA na kujionea shughuli za uendeshaji na baadaye kuelekea Ikulu kwaajili ya mazungumzo.
Rais huyo wa Zambia amewasili nchini siku ya Jumapili na leo ameondoka baada ya kumaliza ziara yake ya kiserikali.