Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo dhamana yake imegoma tena katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kurudishwa tena rumande.
Mbele ya Jaji Fatma Masengi aliyekuwa amepangwa kusikiliza Rufaa hiyo, Upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa na mwanasheria Matenus J Marandu umeweka pingamizi kwamba mawakili wa Lema walipaswa kupeleka notisi ya rufaa kwanza na siyo kukata rufaa
Wakili wa Chadema Peter Kibatala amesema wao wameshakamilisha taratibu zote za kisheria, hivyo wanasubiri uamuzi wa pingamizi hilo lililowekwa na upande wa serikali.
Jaji Fatma Masengi ameutaka upande wa serikali uwasilishe hoja za pingamizi lao kwa njia ya maandishi kabla ya November 30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.