Tume iliyoundwa na Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir kufuatilia mali za Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) imekabidhi ripoti ya awali kwa mufti huyo huku ikiainisha baadhi ya mali za Waislamu zilizoporwa kwa hila.

Hata hivyo, tume hiyo haikuweka wazi mali walizobaini kuporwa na kueleza kuwa jambo hilo litafanywa na Mufti mwenyewe kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za ripoti hiyo.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Shehe Abubakar khalid amesema tume hiyo imefanya kazi kubwa hadi kukamilisha ripoti hiyo ya kwanza.

Shehe Hali amesema tume hiyo ilipewa miezi mitatu, lakini kazi hiyo imekuwa ni ngumu hasa kwa kuzingatia kuwa baraza hilo lina mali nyingi nchini kote na shughuli za tume hiyo ilikuwa ni kuhoji wahusika kwa mikataba waliyoingia. “…Ilikuwa ni tabu kuwapata kwa nafasi zao , tumefanikiwa kukamilisha ripoti ya kwanza kwa baadhi ya mali tu na mikataba ya mkoa wa Dar es Salaam, shughuli nyingine zitaendelea baadaye,” alisema Shehe Khalid na kuongeza kuwa ripoti hiyo waliyowasilisha ni nusu ya ripoti ya awali ya kazi ya Dar es Salaam na wataendelea katika mikoa yote hadi watakapokamilisha na ndio sababu ya kuomba waongezewe muda na wanamshukuru Mufti kwa kuwakubalia jambo hilo kwa kuwaongeza miezi mitatu mingine.

Amesema walipewa hadidu za rejea zilizokuwa zikiwaeleza kufuatilia viwanja, majengo pamoja na mali nyingine zilizokuwa zikimilikiwa na Waislamu na ndilo walilolitekeleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *