Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuanzia sasa hatoweka sahihi kwenye nyaraka yoyote itakayopelekwa katika ofisi yake kabla ya kupeleka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Makonda aMEyasema hayo wakati akizungumza na watumishi katika Manispaa ya Ilala ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya siku mbili katika manispaa hiyo.
Amesema hataweza kusaini nyaraka hizo hadi zitakapochunguzwa kwani amegundua kumekuwa na usanii katika uuzwaji wa viwanja pamoja na kuthaminisha nyumba kwa kuuzwa zaidi ya mara moja huku wananchi wakikosa haki zao kwa kusumbuliwa mara kwa mara.
Makonda ameongeza kuwa wataalamu wa kupima ardhi wamekuwa na tabia ya kuacha maeneo na kudai kuwa ni meneo yenye bonde au mto na kuuza au hata kudai vimeisha kwa manufaa yao na wakati mwingine maofisa hao kubadilisha mafaili ili wauze kwa watu tofauti.
Pia Makonda alisema anafahamu na hatakubali kukaa na watumishi wa vigogo wasioweza kufanya kazi katika mkoa huo huku akiahidi kukagua idara zenye watumishi waliokaa zaidi ya miaka nane.