Mtandao wa kijamii Facebook umetangaza hatua mpya itakazochukuwa kudhibiti taarifa za uongo zinazochapishwa katika mtandao huo.

Mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg amesema yuko katika harakati za kuunda kifaa kipya kitakacho kuwa na uwezo wa kuhakiki taarifa zinazochapishwa kama ni za kweli.

Mtandao wa Facebook umekosolewa kwa kuchapisha taarifa za uongo kuelekea uchaguzi wa urais wa Marekani na huenda ulishawishi matokeo ya uchaguzi huo.

“Tumekuwa tukilishughulikia tatizo hili kwa muda mrefu na tunalitilia maanani sana. “alisema Zuckerberg.

Amesema kuwa matatizo hayo ni magumu. Hata hivyo ameongeza kuwa Facebook haitaki kuzuia ubadilishanaji wa maoni na kuwa kizingiti kwa ukweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *