Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amefunguka na kusema kuwa alimtumia Harmonize ngoma 30 kabla ya kuamua na kutoka na ngoma Naogopa waliofanya wote wawili.
Marioo ametuambia kabla haijatoka ngoma yake ya naogopa alimtumia Harmonzie nyimbo kama 30 kisha akachagua waanze na hiyo.
Amesema kuwa “Nakumbuka nilimsikilizisha Kondeboy Harmonize ngoma kama 30, zote aliwaka nazo mixer kama kudata na yale ma-sound lakini akanambia em tuanze na hii naogopa kwanza”.
“Salute sana my bro najua ngoma ulizochagua zote zitakuwa hits kubwa kama hii au zaidi tuseme Inshaalah”.
Audio ya ngoma hiyo kwa sasa imesikilizwa na watu Milioni 1.6 na video yake imetizamwa mara Milioni 5.6 mtandao wa Youtube mpaka sasa.