Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amemuunga mkono Mwana Fa kutoa saa 48 kwa shirikisho la muziki Tanzania kuhusu nafasi ya usemaji kwa Steve Nyerere.
Kwenye Instagram yake Nay wa Mitego ameandika kwamba watu wasiichukulie kauli hiyo kama ubabe au utemi kwa kutumia nafasi yake kama Mbunge.
“Kauli ya Mwana Fa watu wasiichukulie kama kauli ya kibabe, kitemi na kutumia nafasi yake kama Mbunge lakini haya ni mawazo ya wasanii wengi ambao hawana nafasi ya kuongea na woga wakiamini Steve ni mtu wa ndani na ana-connection. wengi hatuungi mkono maamuzi ya shirikisho, na hiyo ni kauli yetu sio ya Mwana FA”.
“Kama mtu hana sifa za uongozi tukikubali atuongoze ni kama tumekubali bora yaende. yasiwe masaa 48, yawe hata masaa 24. Steve tunakupenda kama msanii wa kuchekesha lakini sio msemaji na afisa mipango wetu”.
Wanamuziki wa Bongo Fleva wameonesha kutokuunga mkono wa Steve Nyerere kuwa msemaji wa Afisa Mipango wa shirikisho la muziki.