Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo amewatunuku Cheo cha Luteni Usu wahitimu 194 wa mafunzo ya Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Hafla ya kutunikiwa vyeo hivyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wahitimu hao kati yao 168 ni wanaume na 26 ni wanawake, kwa ilivyozoeleka miaka ya nyuma walitakiwa kutunukiwa Cheo hicho katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi Monduli na badala yake hafla ya kuwatunuku imefanyika kwenye viwanja hivyo vya Ikulu, Dar.
Wahitimu hao 193 wamehitimu mafunzo hayo katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi Monduli huku mmoja akihitimu masomo hayo nchini Uingereza.
Baada ya kutunukiwa vyeo hivyo wahitimu waliapa kiapo cha utii na kuvalishana nyota kwenye mabega yao huku kila mmoja akimvalisha mwenzake.
Baadaye sherehe zimeendelea viwanjani hapo huku, bras band ya jeshi imetumbuiza na kusherehesha kwa ngoma na matarumbeta yao.